Baada ya Mbeya City kushushwa daraja kwa kufungwa na Mashujaa FC ya Kigoma, Mbunge wa Mbeya Mjini, Dkt. Tulia Ackson amesema kwamba wanajipanga kuhakikisha kuwa timu hiyo inarejea Ligi Kuu Tanzania Bara.
“Niwapongeze Mashujaa kwamba wamefika hiyo hatua na ninawatakia kila la heri. Lakini kwa timu yetu ya Mbeya City tunajipanga vizuri,” amesema Spika Tulia
Amesema timu hiyo haikufanya vizuri msimu huu lakini anaamini kwamba itarejea.