Vumbi lasababisha Bunge kuahirisha kwa muda

Spika Wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Amesema Chanzo Cha Kengele Ya Tahadhari Kulia Bungeni Ni Uwepo Wa Vumbi Lililotokana Na Matengenezo Yanayoendelea Kwenye Moja Ya Vyumba Vilivyo Chini Ya Ukumbi Wa Bunge.

Amesema Matengenezo Hayo Yanahusisha Utinduaji Ambao Umesababisha Vumbi, Hivyo Vifaa Vya Kutambua Hatari Vikainasa Vumbi Hiyo Na Kuitambua Kuwa Moshi, Hivyo Ikapelekea Kengele Kulia.

Amewapongeza Wabunge Wa Kuzingatia Dharura Hiyo Na Kuongeza Kwamba Hakuna Mtu Yeyote Aliyejeruhiwa Wakati Wa Kukimbia Kutoka Nje.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *