Mamlaka ya Mapato Nchini – TRA imesema imejiwekea mikakati mbalimbali, ili kuhakikisha kuwa inaendelea kukusanya mapato ya kutosha kwa lengo la kuiwezesha Serikali kutekeleza mipango ya maendeleo na kuimarisha huduma za jamii kwa watanzania.
Hayo yamesemwa na Kamishna wa TRA, Yusuph Mwenda leo Machi 12, 2025 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma na kuongeza kuwa mikakati hiyo ni kuendelea kujenga na kuimarisha mifumo ya kodi za ndani na forodhi, IDRAS na TANCIS.
Amesema, mifumo hiyo inayosomana na mifumo mingine, inararahisisha shughuli za kiuchumi nchini na kuongeza ulipaji kodi wa hiari pamoja na Kuendelea kuwajengea uwezo wafanyakazi ili watekeleze majukumu yao kwa uadilifu na weledi.

Mwenda amesema TRA imefanikiwa kuongeza watumishi kutoka 4,749 kabla ya mwezi Machi 2021 hadi watumishi 6,989 kufikia mwezi Machi 2025, hii ni sawa na nyongeza ya Watumishi 2,240, sawa na ongezeko la asilimia 47.
“Pamoja na ongezeko hili, Mamlaka ya Mapato inatarajia kuajiri Idadi ya Watumishi 1,596 kufikia mwezi Juni 2025 ambapo zoezi la ajira linaendelea, hizi ni jitihada za Mhe. Rais kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma bora kwa kuiongezea Mamlaka ya Mapato Watumishi wa kutosha ili kuiwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi,” amesema Mwenda.

Aidha ameonfafanua kuwa, ili kuleta usawa katika ulipaji kodi, TRA imeendelea kupambana na wakwepa kodi kwa kuchukua hatua stahiki za kisheria dhidi yao pamoja nakuendelea kutoa elimu ya kodi na madhara ya ukwepaji kodi, baada ya kubaini uwepo wa mianya ya upotevu wa mapato na kuchukua hatua stahiki dhidi
ya wahusika, na kwamba wameongeza uwajibikaji na kuongeza mapato ya serikali.
“Baadhi ya mianya ya ukwepaji kodi ni pamoja uwepo wa magendo kupitia mipaka yetu (uncustomed goods), Ghost receipt za EFD, Counterfeit ETS, Dumping of Transit goods,
Abuse of tax exemptions, Undervaluation of imported goods na Katika miaka mine tumeweza kufungua kesi 77 za ukwepaji kodi katika mahakama mbalimbali pamoja na kurecover kiasi cha kodi kilichopotea,” amesema Mwenda.