TFF, BODI YA LIGI WATOE RIPOTI WALIOHARIBU MCHEZO WA MACHI 8 – SIMBA SC

Uongozi wa Simba SC umewaarifu Wanachama, Wapenzi na Umma kuwa mchezo nambari 184 dhidi ya Yanga SC uliopangwa kufanyika tarehe
15/6/2025 upo kama ulivyopangwa.

Simba SC kupotia taarifa yake ya hii leo Juji 10, 2025 imeeleza kuwa “Tunawasihi msihadaike na kelele za mitaani, Wale ambao walinunua tiketi za mechi ya tarehe 8/3/2025 wazitunze kwa ajili ya matumizi ya mchezo
huo na wale ambao hawajanunua tiketi wajiandae kununua baada ya tangazo la Bodi ya Ligi.”

“Twendeni tukaujaze Uwanja wa Mkapa”
Inafahamika wazi kuwa Ligi Kuu ya NBC inajumuisha Timu 16 na si ligi ya
timu moja, Kwa mujibu wa taratibu kabla ya kuanza msimu, Vilabu vyote 16 hushiriki vikao na kutoa mapendekezo ya kuboresha kanuni na taratibu ili kuimarisha ligi yetu, Hivyo wenye hoja wafuate taratibu husika,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha, Simba pia imeiomba Bodi ya Ligi na TFF kutoa hadharani ripoti ya uchunguzi juu ya wale wote waliohusika kuharibu mechi ya ligi jioni ya tarehe 7/3/2025 na wachukuliwe hatua stahiki na mamlaka husika.

“Kutotolewa kwa ripoti na kutochukuliwa hatua kwa wanaoendelea kuchochea ghasia ni sawa na kulinda uharamia katika mpira ambao unatia dosari mafanikio yaliyopo katika tasnia ya mpira wa miguu nchini
kwa sasa,” ilmeeleza taarifa hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *