TEUZI MPYA ZA RAIS SAMIA: SUSAN KAGANDA BALOZI NCHINI ZIMBABWE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi na kumpangia kituo cha kazi Balozi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa
na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka imeeleza kuwa, Dkt. Fred Matola Msemwa ameteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa
ya Mipango ambapo kabla ya uteuzi huuo alikuwa Afisa Mtendaji Mkuu
wa Watumishi Housing Investments (WHI).

Prof. Philipo Lonati Sanga ameteuliwa kuwa Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu
Wazima (TEWW), na kabla ya uteuzi huo, alikuwa Mhadhiri Mwandamizi katika Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima.

Prof. Sanga anachukua nafasi ya Prof. Michael Ngumbi ambaye amemaliza muda wake, huku Balozi Susan Salome Kaganda akipangiwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe.

Uapisho wa Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango utafanyika kwa tarehe
itakayopangwa baadaye.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *