Staa wa muziki Teni, kutoka Nigeria amelipwa zaidi ya Dola 70,000 sawa na Milioni 175,350,002.99 za Kitanzania kutumbuiza kwenye harusi ya mtoto wa bilionea wa Beninoise, Haija Rissi Razaq Igue
Awali harusi hiyo ilidaiwa ni ya mtoto wa Gavana wa Kwara, ila kwa mujibu wa Afisa Mkuu wa Habari wa Gavana wa jimbo la Kwara, Rafiu Ajakaye, amebainisha kuwa harusi hiyo haikuwa ya mtoto wa Gavana Abdulrazaq bali ya mtoto wa dada yake wa kufikia.