TAKUKURU TABORA YAOKOA MAJAFAFA YA BILIONI 1.4

Na Pascal Tuliano – Tabora.

Taasisi ya kuzuia na kupamba na Rushwa TAKUKURU imefanikiwa kukamata mabelo ya magunia ya kufungia tumbaku yaliyotumika maarufu kama “MAJAFAFA” yapatayo 2,681 yenye thamani ya Shilingi bilioni 1.4.

Akitoa ripoti ya kipindi cha Januari hadi Machi 2025 mbele ya waandishi wa habari katika ofisi za TAKUKURU mkoani Tabora, Azza Mtaita ambaye ni mkuu wa TAKUKURU Tabora amesema zoezi hilo limefanikiwa kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa mkoa, Jeshi la polisi na ofisi ya Mashtaka ya mkoa wa Tabora ambapo magunia hayo yamekamatwa katika operesheni maalum kutoka kwa wafanyabiashara waliokuwa wakiyauza kinyume na utaratibu.

Ameongeza kuwa watuhumiwa katika sakata hilo walifikishwa mahakamani na kufunguliwa kesi kwa mujibu wa sheria.

“Kati ya watuhumiwa hao wapo waliokubali kufanya makubaliano ya kulipa fedha kufidia hasara waliyoisababishia serikali na kurejesha magunia hayo ambayo yamerudishwa ili kugawiwa kwa wakulima kwaajili ya kuhifadhia tumbaku.”

Aidha, TAKUKURU imefanikisha kurejeshwa kwa magunia 1,315 ya tumbaku yaliyotumika kati kati ya 2,681 yaliyokamatwa mabapo magunia hayo yamerejeshwa kwa wakulima kupitia vyama vya msingi vya Mulokhu, Mkombozi, Bukemba Ikobelo na Kasisi, wakati taratibu za ufuatiliaji zinaendelea ili kuhakikisha magunia yaliyosalia yanarudi kwa wakulima kupitia vyama vya msingi kama utaratibu unavyoelekeza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *