Taka za Plastiki Kuyakutanisha Mataifa 175 Canada

Wapatanishi kutoka nchi 175 wanatarajiwa kukutana nchini Canada kuanzia Jumanne ya April 23 ili kuhitimisha maandalizi ya mkataba wa kimataifa wa kukomesha uchafuzi wa mazingira utokanao na plastiki.

Mwaka 2022, mataifa hayo 175 yaliafikiana kukamilisha mkataba huo mwishoni mwa mwaka huu ambao ni mkataba wa kwanza wa Umoja wa Mataifa utakaoshughulikia janga la taka za plastiki zinazopatikana kila mahali huku chembechembe zake pia zikipatikana pia ndani ya damu ya binadamu na hata kwenye maziwa ya mama.

Wapatanishi hao tayari wamekutana mara tatu na wanatarajiwa baada ya mazungumzo ya Ottawa, kufanya duru ya mwisho ya mazungumzo nchini Korea Kusini na Mkutano wa awali uliofanyika Jijini Nairobi Novemba mwaka jana ulikuwa fursa ya kwanza ya kujadili rasimu ya mkataba ambao uliainisha njia za kukabiliana na tatizo hilo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *