Timu ya mpira wa Kikapu ya Boston Celtics imeuzwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni binafsi ya Symphony Technology Group, William Chisholm kwa dola bilioni 6.1.
Kwa mujibu wa Shams Charania wa ESPN anaripoti kuwa mkataba huo wa dola bilioni 6.1 unakuwa ni wa mauzo makubwa zaidi kwa kampuni ya michezo barani Amerika Kaskazini.


Chisholm ni mzaliwa wa Georgetown, Massachusetts na mhitimu wa Chuo cha Dartmouth na shabiki wa maisha ya Celtics, The Boston Globe imeripoti.
