Muigizaji wa filamu ya “Black Panther: Wakanda Forever” Winston Duke(M’Baku,) mwenye asli ya kisiwa cha Trinidad na Tobago, kilichoko kaskazini-mashariki mwa Amerika Kusini, amekula kiapo mbele ya Rais Kagame na sasa ni raia rasmi wa Rwanda.
Kwa mujibu wa wa mitandao wa #TrtAfrika, M’Baku alikula kiapo hicho aliposhiriki makala ya 19 ya sherehe za kumpa jina sokwe maarufu KwitaIzina. Winston Duke na muigizaji mwenza, Danai Gurira, wa filamu maarufu ya Black Panther, waliwapa sokwe majina ya Aguka T’Challa na Intarumikwa yaani jitu mstahimilivu.