SKIMU YA UMWAGILIAJI KUWANUFAISHA WAKAZI WA VIJIJI VINNE MKALAMA

Na Saulo Stephen – Singida.

Mradi wa Skimu ya Umwagiliaji Msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, umeendelea kutekelezwa kwa kasi chini ya usimamizi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji mradi huo wenye thamani ya shilingi bilioni 34.1 unalenga kuwezesha umwagiliaji katika eneo la hekta 800 na kunufaisha zaidi ya wananchi 12,000 kutoka vijiji vinne vya Ishinsi, Ndurumo, Msingi na Kidi.

Hayo yamebainika katika ziara ya Kamati ya Siasa Mkoa wa Singida ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida, Martha Mlatha, Mkuu wa mkoa wa Singida Halima Omari Dendego pamoja na wajumbe wengine ambapo wametembelea katika mradi huo uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Mkoani Singida.

Hadi sasa, utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 50 ambapo baadhi ya kazi muhimu zimeshakamilika, ikiwemo ujenzi wa ofisi ya meneja, barabara ya kuingia bwawani, na sehemu ya mfereji mkuu wa zege huku Changamoto ya muundo wa tuta kutokana na hali ya udongo na maji mengi katika eneo hilo ikiwa imeshughulikiwa kwa kushirikisha wataalamu wa miamba na usanifu wa mabwawa, na kazi zimeendelea kwa kasi.

Wakiiongea kwa nyakati tofauti katika eneo hilo la mradi huo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Marha Mlatha pamoja na Mkuu wa mkoa huo Halima Dendego wamepongeza jitihada zinazofanyika katika utekelezaji wa Mradi huo ambao kukamilika kwake itakuwa ni fursa kubwa kwa wana Mkalama na wana Singida kwa ujumla.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *