Hatua zilizopigwa katika kupunguza vifo vya akina mama wakati wa kujifungua, huenda zikaathiriwa kutokana na kupungua kwa ufadhili wa sekta ya afya Duniani.
Hayo yamebaijishwa na Umoja wa Mataifa (UN), ambayo umesema vifo vinavyotokea wakati wa kujifungua vilipungua kwa asilimia 40 katika kipindi cha mwaka wa 2000 hadi 2023.
Wadau wa sekta ya afya, pia wana hofu ya kupunguzwa kwa ufadhili huo kwa Shirika la Afya Duniani (WHO) lililokuwa linategemea msaada toka kwa Marekani ambayo hivi karibuni imetangaza kusitisha misaada ya nje kutaleta athari.

Mwaka 2023, kila baada ya dakika mbili takriban Wanawake 260,000 walifariki kutokana na changamoto za uzazi.
Ikumbukwe pia hivi karibuni, WHO nayo ilionya kwamba kupunguzwa kwa ufadhili wa sekta ya afya duniani, kutasababisha vikwazo katika vita dhidi ya maambukizo ya kifua kikuu na Ukimwi.