Na Saulo Stephen – Singida.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Martha Mlata, ameipogeza Serikali kwa kutoa Fedha na kusimamia matumizi yake ipasavyo kwa ujali ya utekelezaji wa miradi ya Maendeleo mkoani Singida.
Mlatha ametoa kauli hiyo akiwa kwenye ziara ya Kamati siasa Mkoa wa Singida katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida vijijini ambapo kamati hiyo imekagua ujenzi wa Jengo la utawala katika Halmashauri hiyo na Mwenyekiti huyo wa CCM mkoa wa Singida kuridhishwa na Mradi huo ikiwa ni pamoja kuwataka watendaji kuendelea kusimamia fedha za miradi ya maendeleo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Omari Dendego amewataka watendaji katika Halmashauri hiyo kumtumia Katibu tawala Mkoa wa singida katika kurahisisha upatikanaji wa Fedha za miradi ya maendeleo na kuacha tabia ya kwenda kufatilia fedha hizo Dodoma na kutokwenda kwa mtendaji wa mkoa ambae ni katibuTawala.