Kupitia ukurasa wao wa Mtandao wa Kijamii, Singida Black Stars SC wametia neno kuhusiana na sakata la kuandamwa kwa Ladarck Chasambi, wakidai mchezaji huyo hataki magoli ya dhuluma.
Utani huo wa Singida BS unakuja kufuatia Winga huyo wa Simba SC kujifunga na kuisawazishia Fountain Gate katika mtanange ulioisha kwa sare pacha ya 1-1 katika uwanja wa Kwaraa, uliopo mjini Babati Mkoani Manyara.


“Mnamtukana bure tu mwenzenu hataki magoli ya dhuruma kaona asawazishe maana goli lenyewe mlilo funga lilikua off side. Kingine Nyie uwanjani mlikua 14 wachezaji 11 malanzimeni wawili 2 na refa Mmoja 1 lakini wakashindwa kushinda dhidi ya fountain gate walioko 9 uwanjani!,” linasomeka andiko hilo la Singida BS.
Timu hiyo ya Singida BS, hii leo itaingia dimbani kupimana nguvu na Kagera Sugar katika uwanja wa Liti mjini Singida.