Shambulizi la Isarel Laua 37 Gaza

Takribani watu 37 wameuawa katika shambulizi la bomu lililofanywa na Israel katika shule inayosimamiwa na UN katika Ukanda wa Gaza ambayo jeshi la Israel linadai ilikuwa ni maficho ya kundi la wanamgambo la Hamas.

Jeshi la Israel limesema limewaangamiza wanamgambo kadhaa kupitia shambulio hilo waliokuwa ndani ya shule hiyo inayosimamiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi wa Kipalestina,katika eneo la Nuseirat katikati mwa Ukanda wa Gaza.

Israel inalishtumu kundi la Hamas na washirika wake huko Gaza kwa kutumia shule, hospitali na miundombinu mingine ya kiraia ikiwa pamoja na vituo vinavyoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi kama vituo vya operesheni zake, madai ambayo yamekanushwa na kundi hilo.

Wakati huo huo hii leo Hispania limekuwa taifa la pili la Umoja wa Ulaya baada ya Ireland kujiunga na kesi ya Afrika Kusini dhidi ya Israel katika mahakama ya ICC. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *