
Mabehewa 264 ya mizigo ya reli ya kisasa (SGR) yapo katika Bandari ya Dar es Salaam na Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema linatarajia kuanza kusafirisha mizigo kati ya Januari hadi Machi mwaka 2025.
Mkurugenzi Mkuu wa TRC, Masanja Kungu Kadogosa amesema kazi ya kuyashusha mabehewa hayo tayari imeanza na mwezi ujao wataanza kusafirisha mizigo hadi Dodoma kwa awamu ya kwanza.
Kadogosa amewataka Wafanyabiashara kuingia mkataba na shirika hilo pindi treni ya mizigo itakapoanza ili kuhakikisha mizigo yao inafika kwa muda na siku iliyopangwa.
Aidha Kadogosa aliongeza kwa kusema treni ya mizigo itakapoanza hawatachukua mizigo inayobebwa na malori, badala yake watajenga bandari kavu ambayo itakuwa kituo cha kushusha mizigo hiyo na malori kuipeleka katika maeneo husika.