Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Serikali mkoani Simiyu yagundua zahanati bubu inayofanya kazi na waataalamu wasio na taaluma ya udaktari

Serikali Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu imebaini uwepo wa zahanati bubu katika Mtaa wa Giriku uliopo Kata ya Bunamhala, Wilayani humo ambayo inatoa huduma za matibabu kwa wakazi wa mtaaa huo ikiwemo akina mama wajawazito wakati wa kujifungua licha ya mtoa huduma wa zahanati hiyo kutokuwa na utaalamu wa kazi hiyo, hali iliyosababisha kifo cha mtoto mchanga baada ya kushindwa kumsaidia mama mmoja aitwaye limi polole (35) aliyefika katika zahanati kwa ajili ya kujifungua.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Simon Simalenga amefika katika eneo hilo, lililokuwa likitumika kuhudumia wagonjwa pasipo kufuata utaratibu na kutoa maelekezo ya serikali ya kufungwa kwa zahanati hiyo na kufikishwa mahakani kwa wote wanaohusika na tukio hilo.

Kwa Upande wake Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Dk. Judith Ringia amesema mama huyo alijifungua mtoto akiwa tayari ameshafariki kutokana na mazingira hafifu na yaliyo chini ya kiwango pamoja na mtoa huduma ambaye hana taaluma yoyote ya udaktari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *