Klabu ya Soka ya Real Madrid inaangalia uwezekano wa kufunga dili la kumsajili beki wa kulia wa Liverpool Trent Alexander-Arnold kama mchezaji huru msimu wa joto.

Trent ni mmoja wa wachezaji watatu muhimu pamoja na mfungaji bora wa Premier League Mohamed Salah na nahodha wa klabu Virgil van Dijk – ambao muda wao uliopo Anfield unaisha majira ya joto.