Jambo La Leo

Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

RC Mndeme atembelea Banda la Jambo Media SBF

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme ameipongeza Jambo Media kwa kuhabarisha na kuwafikia wananchi kupitia matangazo yake kwenye mitandao ya kijamii, tovuti pamoja na vipindi vyake vinavyoruka kila siku.

Mndeme ameeleza hayo leo Novemba 24, 2023 wakati akikagua banda la Jambo FM katika kongamano la biashara lililoanza leo na kutarajiwa kutamatika Novemba 26 mwaka huu katika viwanja vya Karena hotel na kuwasisitiza wananchi kuendelea kusikiliza Jambo Fm na kuichukulia kama fursa ya kuwekeza kibishara zaidi.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amepongeza bidhaa zinazozalishwa na kiwanda cha Jambo na kuwafikia walaji pamoja na kuwasihi wakazi wa Mkoa wa Shinyanga kuwa na desturi ya kuwa wazalendo kwa kupenda vya nyumbani.

Kongamano hili la biashara litakalofanyika kwa siku tatu limeandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa chini ya Mkuu wa Mkoa Christina Mndeme kwa kushirikiana TCCIA, Jambo Group, Jambo Fm pamoja na wadau na taasisi mbalimbali za biashara mkoani Shinyanga lililolenga kuwapa nafasi wafanyabiashara kueleza changamoto zinazowakabili na kutafutiwa ufumbuzi kwa wakatI.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *