Na Eunice Kanumba,Shinyanga
Wakati Shamra shamra za maadhimisho ya wiki ya viziwi kitaifa zikiwa yanaendelea katika mkoa wa Shinyanga, mkuu wa mkoa huo Anamringi Macha amewaagiza Wakurugenzi wa halimashauri zote za mkoa huo pamoja na Wakuu wa Taasisi kuhakikisha maafisa Habari, na Mawasiliano, wanapatiwa mafunzo ya lugha ya alama ili waweze kusaidia mawasiliano katika utoaji wa huduma kwa makundi maalum.
RC Macha ametoa agizo hilo wakati akifungua Maadhimisho ya Wiki ya Viziwi Duniani ambayo yalianza tarehe 23 Septemba, 2024 yanayotarajiwa kuhitimishwa September 28 huku akisisitiza kuwa lugha ya alama ni sawa na lugha nyingine zinazotambulika kimatifa.
“Nawaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri na Taasisi zote ndani ya Mkoa huu kuhakikisha wanawapeleka mafunzoni Maafisa Habari, Mawasiliano, Itifaki na Uhusiano ili waweze kusaidia mawasiliano na utoaji wa huduma kwa wananchi na hasa makundi maalum wakiwemo viziwi kwani hawa ni wenzetu na wanazo haki zote kama binadamu wengine,” amesema RC Macha”
Kwa upande wake katibu Tawala mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni ameelezea utaratibu na ratiba ya maadhimisho hayo kuwa yameanza tangu tarehe 23 Septemba, 2024 na yatahitimishwa rasmi tarehe 28 Septemba, 2024 ambapo yanatarajiwa kufungwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete.
Awali akitoa salamu za Chama cha Viziwi Tanzania Mwenyekiti mwenyekiti wa chama hicho Celina Mlemba amesema kuwa, maadhimisho haya ni utekelezaji wa Azimio la Umoja wa Mataifa la tarehe 9 Disemba, 1917 la kuzitaka nchi wanachama kufanya maadhimisho ya Wiki ya Viziwi Duniani kila ifikapo wiki ya mwisho wa mwezi Septemba ya kila mwaka ambapo kauli mbiu kwa mwahuu inasema “ungana kutetea haki ya lugha za alama”