RC MACHA AWAPA TANO WAFANYABIASHARA KWA KUTOPANDISHA BEI ZA BIDHAA KIPINDI CHA MFUNGO

Na Eunice Kanumba – Shinyanga.

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha  amewashukuru wafanyabiashara katika  mkoa wa Shinyanga ambao awali katika kuanza kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani na kwaresima aliwaomba kutokupandisha bei za bidhaa hasa vyakula  pamoja na nafaka  kwa lengo la kujipatia faida Zaidi jambo ambalo amesema wamelizingatia na hivyo hapakuwa na mfumuko wa bei katika kipindi chote

RC Macha ameyasema hayo alipojumuika kupata iftari na watoto wenye mahitaji maalum,viongozi wa dini pamoja na vyama vya siana hafla iliyofanyika nyumbani kwake ambapo pia ametumia fursa hiyo kumuombea dua rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr Samia Suluhu Hassan ili awe na afya njema maisha marefu yenye Baraka Zaidi ili aendelee kuwatumikia wananchi wote wakiwemo wana Shinyanga.

RC Macha ametumia fursa hiyo   kuwashukuru viongozi wote kwa dua hiyo njema ya kumtaki kheri    Rais  Samia na kuwataka kuendelea kuliombea taifa pia hususa katika kipindi cha kuelekea katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

“Ninawashukuru sana viongozi wote wa dini  vyama vya siasa na watoto wetu wenye mahitaji maalum kwa kufanya dua hii maalum ya kumuombea Rais Dr Samia Suluhu Hassan afya njema, kheri, baraka, maisha marefu na nguvu zaidi ili aweze kuendelea kuwahudumia Wanashinyanga na Watanzania wote kwa ujumla,” amesema RC Macha.

Hafla hiyo ya Iftar pamoja na Dua hii Maalum ya kumuombea  Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imejumuisha    Watoto wote  wenye Mahitaji Maalum kutoka maeneo mbalimbali ya hapa Manispaa ya Shinyanga ili kuwawakilisha watoto walioko katika maeneo mengine ya mkoa wa Shinyanga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *