RC Macha Aguswa na Mchango wa Jambo Group Katika Maendeleo ya Mkoa wa Shinyanga

Hii Leo Mei 14,20204 kupitia mahojiano maalum akiwa ofisini kwake,Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha ameipongeza Kampuni ya Jambo Group of Companies kwa uamuzi wa kuwekeza katika mkoa wa Shinyanga akielezea kwamba uwekezaji huo  umefungua fursa mbalimbali ikiwemo ajira.

RC Macha ameelezea kuridhishwa na kuutambua mchango wa Jambo Group ambao umekwenda mbali zaidi hadi katika sekta ya Michezo kwa kuwezesha udhamini kwa timu ya Stand United.

“Kwa Shinyanga,Specific kwa wilaya ya Shinyanga ambayo ndio makao makuu ya mkoa hakuna development ya viwanda na mtu anaweza kuja kuangalia mazingira ya hapa na akawa na mashaka kuweka viwanda lazima tukiri ni mji mzuri sana lakini haujawa very well combined katika viwanda,hakujawa na bishara nyingi za kutosha as a kiwanda lazima tuone Jambo as  Giant Industries kama kampuni yenye viwanda vingi hivyo tupongeze na ndani ya viwanda hivi kuna ajira na kuna mapato ya Serikali”Amesema RC Macha.

Akizungumza kuhusiana na ushirikiano na Jamii pamoja na  kujali wafanyakazi,RC Macha  amesema kutoa zawadi kwa wafanyakazi kupitia sikukuu ya Mei Mosi,malipo ya stahiki za wafanyakazi kwa utaratibu unaostahili,kuzingatia usalama wa wafanyakazi  ni mambo yanayopatikana katika viwanda vichache vya binafsi na ni kielelezo cha utendaji bora na kuahidi kushirikiana na Jambo Group katika kuhakikisha timu ya Stand United inaeendelea akiamini kwamba timu hiyo ikisimamiwa vizuri na kuwa na uongozi imara itawezesha kuuchangamsha mkoa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *