Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, anatarajia kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Daraja la Kigongo-Busisi JPM Magufuli June 19 mwaka huu daraja linalotajwa kua kichocheo cha uchumi wa Tanzania na nchi Jirani
Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulegawakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika hafla iliyofanyika katikati ya daraja hilo alipokua akielezea kazi zilizotekelezwa ndani ya kipindi cha miaka minne ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita.

Aidha, amebainisha kuwa Serikali chini ya Wizara ya Ujenzi imefanikiwa sana kwenye ujenzi wa madaraja, barabara, vivuko na kurahisisha utoaji wa huduma kwa jamii pamoja na kukuza uchumi wa watanzania.
Ulega amesema Daraja hilo limejengwa na kampuni ya China Civil Engineering (CCECC) kwa Shilingi Bilioni 716 ni la kwanza Afrika Mashariki na kati likiwa na urefu wa Kilometa tatu na urefu wa mita 17 kutoka usawa wa bahari na litakuwa na uwezo wa kupitisha magari 20,000 kwa siku moja huku likiwa na uwezo wa kupitisha magari yenye uzito wa tani 160 za mizigo kwa pamoja.

Katika hatua nyingine waziri Ulega amesema Ras Samia amefanya kazi kubwa ya kuhakikisha ndoto hiyo iliyoasisiwa na Hayati John Magufuli inakamilika kwani wakati huo lilikuwa limetekelezwa kwa asilimia 25 pekee na zaidi ya Sh200 bilioni zikiwa zimelipwa, hivyo, imefanyika kazi kubwa kuhakikisha zaidi ya Sh500 bilioni zilizokuwa zinahitajika zinapatikana kukamilisha mradi huo.
Sambamba na madaraja amefafanua kuwa mtandao wa barabara umeongezeka kutoka Kilomita elfu 36 hadi 37. 4 kutokana na kupandishwa kwa hadhi ya barabara kutoka wilaya kwenda kuwa za mikoa huku akizitaja barabara za Mbambabay (KM 66), Kigoma-Kasulu (KM) 100.