Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Polisi wajipanga kupunguza matukio ya ukatili 2024

Takwimu zinaonyesha kundi la watoto limeathiriwa zaidi na matukio ya ukatili hasa ubakaji na ulawiti kwa mwaka 2023, ambapo dawati la jinsia mkoa wa Shinyanga limeahidi kuendelea kusimamia mwongozo na utoaji wa elimu kwa umma juu ya ukatili wa kijinsia ili kuendelea kuwajengea uelewa wananchi katika kuendeleza vita ya kupinga ukatili kwa mwaka 2024.

Hayo yameelezwa na mkaguzi msaidizi wa jeshi la polisi ambaye pia ni mkuu wa dawati la jinsia wilaya ya Shinyanga Jane Mwazembe wakati akizungumza na Jambo Fm kuhusiana na mikakati ya jeshi hilo katika kupunguza au kumaliza kabisa tatizo la ukatili wa kijinsia katika mkoa wa Shinyanga.

Katika hitimisho la siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa mwaka huu ambazo zilianza November 25 hadi December 10 Mwazembe amesema katika msimu huu hukukuwa na matukio ya ukatili ya kutisha tofauti na miaka ya nyuma na kusema hayo yote ni matokeo ya elimu inayotolewa na jeshi hilo katika jamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *