Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Picha:Kampuni ya Jambo Food Products yaingiza bidhaa mpya sokoni, ni ‘Mkate wa Nazi

Kampuni inayojishughulisha kuzalisha na kuuza bidhaa mbalimbali za vyakula na vinywaji mkoani Shinyanga Jambo Food Products rasmi imezindua na kutambulisha mwanafamilia mpya kutoka Jambo Bakery ambaye atatumika kwa matumizi ya mlo kukupa nguvu, kuimarisha mifupa na faida nyingi za afya kila unapotumika.

Mwanafamilia huyo mpya ametambulishwa kwa jina la Jambo Coconut Bread yaani mkate wa nazi ambao umetengenezwa kwa kutumia nazi halisi na ni mlaini ambao unatumika kwa kinywaji cha aina yoyote ikiwemo chai, maziwa, maji, kahawa na sharubati {juice}.

Mkate huo unapatikana kwa bei nafuu kabisa kwa kuzingatia hali ya wananchi kwa size tofauti tofauti ambapo mkate mdogo wa gram 400 unauzwa kwa kiasi cha shilingi 1500 na mkubwa wa kilogram 1 kwa shilingi 4000 unaopatikana katika maduka yote mkoani shinyanga. Aidha kwa kujali na kuthamini wateja wa bidhaa kutoka Jambo Food Products kampuni hiyo inauza mkate huo kwa bei ya punguzo kwa siku saba kuanzia tarehe 13 hadi tarehe 20, ambapo mkate mdogo unapatikana kwa shilingi 1200 badala ya 1500 na mkate mkubwa kwa shilingi 3000 badala ya shilingi 4000.

Mmoja kati ya Wakurugenzi wa Kampuni wa Jambo Group Bwn. Nassor Salum Khamis( Wapili kutoka kulia) na Meneja Mkuu wa Jambo Media, Bwn. Nickson George((Wapili kutoka kushoto) na Wawakilishi kutoka Jambo Bakery wakimkaribisha rasmi mwanafamilia mpya wa kifungua kinywa chetu ambaye ni Mkate wa Nazi kutoka Jambo Group.

 Meneja Mkuu wa Jambo Media, Bwn. Nickson George  akiwa ameshikilia mkate wa Nasi kutoka Jambo.

Mmoja kati ya Wakurugenzi wa Kampuni wa Jambo Group Bwn. Nassor Salum Khamis na Meneja Mkuu wa Jambo Media, Bwn. Nickson George na Wawakilishi kutoka Jambo Bakery wakimkaribisha rasmi mwanafamilia mpya wa kifungua kinywa chetu ambaye ni Mkate wa Nazi kutoka Jambo Group.

Meneja Mkuu wa Jambo Media, Bwn. Nickson George  akitoa maelekezo kwaajili ya kumpokea Mwanafamilia mpya wa kifungua kinywa chetu ambaye ametambulishwa rasmi leo kwenye Power Fresh, huyu si mwingine bali ni Mkate wa Nazi kutoka Jambo Group.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *