PAPA MPYA NI LEO XIV, MAKADINALI WAMALIZA KAZI

Kanisa Katoliki Duniani, limemtangaza Kiongozi wake mpya, Papa Leo wa 14 baada ya uchaguzi uliofanywa na makadinali wapatao 133 kutoka mataifa 70 Ulimwenguni.

Papa Leo XIV, ambaye jina lake ni Robert Francis Prevost, alizaliwa Chicago Septemba 14, 1955 na alisoma katika Chuo cha Kitheolojia wa Kikatoliki wa Chicago, na kutunukiwa diploma.

Akiwa na umri wa miaka 27, alisomea sheria za kanuni katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Mtakatifu Thomas Aquinas (Angelicum) cha Roma, na baadaye alifika Peru kama mmishionari na kushika nyadhifa mbalimbali huko Marekani na Peru.

Alifahamiana na Papa Francis katika nchi hiyo ya Amerika Kusini na mwaka 2023 akamteua kuwa mkuu wa Baraza la Maaskofu na kumfanya kuwa Kardinali.

Katika jukumu hilo, amehusika na uteuzi wa maaskofu duniani kote kwa miaka miwili, huku akiwa ni rais wa Tume ya Kipapa ya Amerika ya Kusini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *