ODINGA AUKOSA UENYEKITI AUC, DJIBOUTI WATAMBA

Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Odinga ameshindwa katika kinyang’anyiro cha mgombea Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC), nafasi ambayo imechukuliwa Waziri wa Mambo ya nje wa Djibouti, Mahamoud Ali Youssouf.

Mahamoud ameshinda Raila Odinga ambaye alikuwa mwakilishi pekee kutoka Afrika Maahariki, aliyeongoza duru mbili za kwanza na kupoteza katika mzunguko wa tatu.

Katika awamu ya kwanza, Odinga alipata kura 22 huku Mahamoud akipata kura 18 na Randriamandrato alipata kura 10 na awamu ya pili, Odinga alipata kura 20, Mahamoud 18, na Randriamandrato 10.

Hata hivyo, Mahamoud alimshinda kwenye awamu ya tatu kwa kura 23 dhidi ya 20 za Raila Amolo Odinga (79), Kiongozi wa upinzani nchini Kenya aliyekuwa akipewa nafasi ya kushinda nafasi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *