NTOBI WA CHADEMA AFUNGUKA BAADA YA KUVULIWA UENYEKITI….

NA EUNICE KANUMBA –SHINYANGA

Baada ya Kamati Tendaji ya CHADEMA Kanda ya Serengeti kumvua uenyekiti Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Ntobi, kufuatia tuhuma za kimaadili alizokuwa akituhumiwa nazo, ikiwemo kuwatukana viongozi wa kitaifa katika mitandao ya kijamii.

Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chadema Kanda ya Serengeti Lucas Ngoto ameiambia jambo media kuwa maamuzi hayo ya Kikao yamefikiwa Kisheria ikiwa ni mara baada ya kumpa fursa ya kuweza kujitetea dhidi ya kauli na maandiko yake kadhaa yasiyokuwa na utu na heshima kwa Viongozi wa Chama Taifa.

Aliyekua Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Shinyanga Emmanuel Ntobi amekana tuhuma dhidi yake na kusema kuwa hatua hiyo ni matokeo ya “joto la kisiasa” kutokana na msimamo wake wa kumuunga mkono Mwenyekiti wa sasa wa chama  hicho Taifa Freeman Mbowe, anayewania nafasi ya Uenyekiti wa CHADEMA Taifa kwa awamu nyingine tena.

Ntobi amefafanua kuwa  hatua hiyo ni “ajali ya kisiasa” inayotengenezwa na wafuasi wa Tundu Lissu, ambao kwa madai yake ni baadhi ya viongozi wameungana kumchukulia hatua kinyume cha taratibu.

“Sijapelekwa kwenye kamati ya maadili, hili ni joto kubwa la kisiasa kufuatia uchaguzi unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni, nimeonewa kwa sababu ya joto la kisiasa” amesema Ntoby

Ntobi ambaye pia mwaka 2023 aliwahi kusimamishwa Uenyekiti wake kwa mwaka mmoja kutokana na makosa ya kinidhamu, amejitanabaisha mitandaoni  kuwa anamuunga  mkono mwenyekiti anayetetea nafasi yake katika uchaguzi wa cha chama hicho ngazi ya taifa Freeman Mbowe ambapo kufukuzwa kwake kumeibua hisia kubwa miongoni mwa makundi mawili yanayokinzana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *