Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Naibu Waziri Stanslaus Nyongo mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya siku ya idadi ya watu duniani julai 11, 2024 Mkoani Geita

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Stanslaus Nyongo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho siku ya idadi ya watu duniani inayotarajiwa kufanyika Julai 11, 2024 huku maadhimisho hayo kitaifa yakitarajiwa kufanyika Mkoani geita katika viwanja vya Epza Bombambili Mjini Geita.

Hayo yamebainishwa na Afisa Mipango kutoka Tume ya Mipango Zanzibar Umrat Mohamed wakati akizungumza na wandishi wa habari katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita ambapo amesema maadhimisho hayo yatatumika kama njia moja wapo ya kutoa elimu mbalimbali kwa vijana pamoja na wakazi wa Mkoa wa Geita juu ya umuhimu wa uzazi wa mpango pamoja na faida za matumizi sahihi ya takwimu za idadi ya watu katika kujiletea maendeleo binafisi.

Naye Mchambuzi wa Idadi ya Watu na Maendeleo kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (Unfpa) Ramadhan Hangwa amesema maadhimisho hayo yanafanyika kitaifa Mkoa wa Geita kutokana na Mkoa huo kukua kwa kasi ya ongezeko la watu la asilimia 5.4 ikilinganishwa na asilimia ya ukuaji wa nchi wa asilimia 3.2.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *