MZEE WASIRA ATEULIWA MAKAMU MWENYEKITI CCM…..

Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imewasilisha jina la Stephen Wasira kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM, Wasira ambaye ni Mwanasiasa aliewahi kushika nafasi mbalimbali katika Serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Jina la Mzee Wasira limewasilishwa mbele ya mkutano mkuu wa CCM unaoendelea jijini Dodoma leo Januari 18, 2025 na kupata baraka za Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Abdulrahman Kinana aliyetangaza kupumzika miezi michache iliyopita mwaka jana (2024).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *