Watanzania wametakiwa kupunguza unywaji wa pombe ili kuepuka magonjwa yasiyoambukiza,
Kwani sababu kubwa ya kuongezeka kwa magonjwa hayo ni matumizi makubwa ya unywaji pombe.
Hayo yamesemwa na waziri wa afya Ummy Mwalimu wakati akizindua kampeni ya kuelimisha jamii juu ya magonjwa yasiyoambukiza ambapo katika hatua nyingine amesema ugonjwa wa Saratani umeongezeka kwa kasi mwaka 2020 ambapo umeonesha vifo vipya zaidi ya 40,000 ukiongozwa na Saratani ya Mlango wa Kizazi.
“Takwimu zinaonesha Tanzania ni nchi ya tatu kwa matumizi ya pombe barani Afrika ikiongozwa na Uganda.”Amesema na kuongeza
“Hatusemi msinywe pombe, lakini tunasema mpunguze unywaji wa pombe kupita kiasi, takwimu za Shirika la Afya Duniani zinaonesha Tanzania Watu kuanzia umri wa miaka 15 na kuendelea kwa mwaka tunakunywa Lita 10.4 za pombe.” Amesema na kuongeza.