MLULU JELA MIAKA 20 KWA KUMILIKI SILAHA BILA KIBALI

Mahakama ya Wilaya ya Kasulu imemhukumu Timotheo Mlulu Rumambo, mwenye umri wa miaka 28 Mkulima wa Kitanga Wilaya ya Kasulu, kifungo cha miaka 20 jela kwa kosa la kupatikana na silaha ya moto.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa mahakamani, mshtakiwa alikamatwa tarehe Mei 5, 2024 huko maeneo ya makere (south forest reserve Wilaya ya Kasulu, Mkoa wa Kigoma na kikosi maalum cha kupambana na ujangili (Task Force), akiwa na silaha ya moto aina ya gobole.

Hakimu Mkazi Mwandamizi, Mwakitalu, alitoa hukumu hiyo Juni 3, 2025 baada ya kuridhishwa na ushahidi uliowasilishwa Mahakamani dhidi ya mshtakiwa
pia alieleza kuwa kitendo cha kumiliki silaha bila kibali ni kosa kubwa na la kuhatarisha usalama wa jamii na uhifadhi wa mazingira.

Aidha, Mheshimiwa Mwakitalu alibainisha kuwa adhabu hiyo iwe fundisho kwa wananchi wengine, hasa wale wanaojihusisha na vitendo vinavyokiuka sheria, ikiwemo ujangili na umiliki wa silaha haramu katika maeneo ya hifadhi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *