MLINDA MLANGO HARAMBEE STARS AANGUSHIWA JUMBA BOVU

Shirikisho la Soka Nchini Kenya (FKF), linafuatilia ukweli wa picha mjongeo, ambayo haijafahamika mara moja ni ya lini, ikimuonesha Mlinda mlango wa Timu ya Taifa ya soka, Harambee Stars na Klabu ya Kakamega Homeboyz, Patrick Matasi na watu wasiojulikana wakipanga kuhujumu matokeo ya mechi kadhaa za soka.

Mbali na kwamba FKF inafuatilia, tayari kumeibuka mjadala mkali Nchini humo, licha ya kuwa bado haijawekwa wazi ni akina nani waliokuwa kwenye picha mjongeo hiyo na hata kujulika ni lini na wapi ilirekodiwa.

Kipa huyo, amekuwa akisemwa vibaya kutokana na kufungwa magoli rahisi wakati akiichezea Timu ya Taifa na Klabu yake na FKF limeanzisha uchunguzi na kudai litachukua hatua kwa mujibu wa sheria za FIFA na CAF.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *