Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Mbunge wa Nyamagana, Stanslaus Mabula atatua changamoto ya madawati katika shule mbili

Kutokana na changamoto ya Madawati ambayo ilikua inawakabili wanafunzi wa shule ya sekondari Mlimani pamoja na wale shule ya sekondari Bugarika, Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza Stanslaus Mabula ametoa jumla ya madawati 50 kwa kila shule ili kuwanusuru wanafunzi kukaa chini kutokana na upungufu wa madawati.

Akitoa madawati hayo Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza Stanslaus Mabula amesema serikali inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imejenga vyumba vya madarasa kwa mfumo wa ghorofa katika shule mbali mbali za jijini Mwanza hivyo ni vyema kila vyumba vya madarasa vikawa na madawati ya kutosha kwa ajili ya wanafunzi.

Kwa upande wake Afisa Elimu sekondari Halmashauri ya Jiji la Mwanza Hakimu Mafuru pamoja na mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mlimani Jodani Mbokwa wamempongeza mbunge wa Jimbo la nyamagana kwa kutoa madawati hayo kutokana na upungufu wa madawati uliopo ambapo kwasasa itawasaidia wanafunzi kupata Elimu kwa ufanisi wa Hali ya juu.

Nao baadhi ya wanafunzi waliopata madawati hayo wameishukuru serikali ya Rais Samia pamoja na Mbunge wa Jimbo hilo la Nyamagana kwa kuwaletea madawati katika shule zao kwani yanakwenda kupunguza tatizo la upungufu wa madawati lililokua linawakabili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *