Serikali imefanikiwa kupunguza idadi ya vifo vya akina mama wajawazito na Watoto wachanga kutoka 556 kwa kila vizazi hai 100,000 kwa mwaka 2016 hadi kufikia 104 kwa mwaka 2022 kufuatia ukuaji wa teknolojia ikiwemo kitita cha uzazi salama.
Hayo yamebainishwa na mkurugenzi wa huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais – TAMISEMI Dkt. Rashid Mfaume alipotembelea Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana mkoa wa Mwanza akiwa ameongozana na timu ya Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI.
“kabla ya hizi teknolojia wakati mwingine mtoto anazaliwa hauoni kifua kikiwa kinacheza inaweza kusema mtoto amefariki kwasababu huoni kama anahema lakini wengine tulikwa tunatumia teknolojia za zamani kuangalia mapigo ya moyo ya mtoto kwa kugusa kifuani kumbe kuna mapigo ya moyo huwezi kuyasikia Zaidi ya teknolojia ambayo imethibitishwa ambayo inaweza ika’peack’ baadae ukamsaidia mtoto aheme” amesema Dkt. Mfaume.