MAHAKAMA YAFUTA KESI ZA ACT KUPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

Mahakama ya Wilaya ya Kigoma, imetupilia mbali kesi zote nne
zilizokuwa zimebaki kati ya 11 zilizofunguliwa na Wanachama wa ACT
Wazalendo, kupinga matokeo ya uchaguzi wa Serikali za mitaa katika
mitaa mbalimbali ya wilaya hiyo.

Akisoma hukumu ya kesi iliyomuhusisha aliyekuwa mgombea wa Uenyekiti wa Mtaa wa Kibirizi, Didas Baoleche wa ACT Wazalendo na Mrisho Mwamba wa CCM, Hakimu mfawidhi wa Mahakama hiyo, Ana Kahungu amesema mlalamikaji Baoleche ameshindwa kuwasilisha baadhi ya vielelezo vinavyoonyesha kuwa uchaguzi katika mtaa huo haukuwa huru na wa haki.

Amesema, “ipo wazi na hapakuwepo na Ushahidi au vielelezo vinavyo muonyesha kuwa mlalamikaji aliteuliwa na msimamizi wa uchaguzi kuwa mgombea wa nafasi hiyo ya umwenyekiti ambapo katila utetezi wa mlalamikiwa alidai kuwa mlalamikaji hakuteuliwa kugombea nafasi hiyo na ni kweli hakuna barua wala uthibitisho wowote juu ya uteuzi wake.”

Aidha, Kahungu amesema mlalamikaji ameshindwa kuithibitishia mahakama juu ya madai ya uwepo wa kura badia alizozishuhudia zikiwekwa kwenye Sanduku la kura siku ya upigaji kura na kwamba feki zilikuwa ngapi na halali zilikuwa ngapi ili mahakama ijiridhishe.

Kwa upande wake wakili Luta Kivilo, ambaye amesimamia kesi hiyo
amesema wanampango wa kukata rufaa katika mahakama za juu ili
kuendelea kuitafuta haki ya wateja wake kisheria.

Amesema, “tulikuwa na Jumla ya Kesi 11 tulizofungua katika Wilaya ya Kigoma
kupinga matokeo ya serikali za mitaa ambao ulifanyika Tarehe 27
Novemba 2024 katika kesi hizo kesi nne Zilitupiliwa mbali katika hatua
ya kwanza ya Mapingamizi tukawa tumebakiwa na kesi saba ambapo
kati ya hizo moja tulishinda na Sita tumeshindwa tumepokea maamuzi
ya mahakama kama ilivyo amua.”

Aidha, Kivilo amesema anatarajia kukutana na wateja wake ili kwanza
taratibu za kukata rufaa Kwenye mahakama za juu ili kuendelea
kuitafuta haki ya wateja wake Kisheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *