Rais wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwepo Dubai kwa ajili ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28), ameamua kufupisha safari hiyo na kurejea nchini haraka iwezekanavyo ili kushughulikia kwa karibu janga la mafuriko Wilayani Hanang ambalo limesababisha vifo vya zaidi ya Watu 50 na zaidi ya 80 kujeruhiwa.
Janga hilo licha ya kusababisha vifo na majeruhi limefanya pia Watu wengine wahofiwe kuwa bado wamefukiwa na tope baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko na maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha Wilayani humo ambapo juhudi za uokoaji zinaendelea.