LISSU KUSIMAMIWA NA MAWAKILI WA NDANI YA NCHI NA NJE YA NCHI – CHADEMA.

Makamu Mwenyekiti wa Chadema bara, Mhe. John Heche amesema kuwa Chama hiko tayari kimewapata Mawakili wa kusimamia kesi ya Mwenyekiti wa chama chao Taifa, Mhe. Tundu Lissu pindi akifikishwa mahakamani.

Heche amesema mawakili wao wa ndani na nje ya nchi wakiongozwa na Robert Amsterdam tayari wamepewa taarifa kamili kuhusu kukamatwa kwa mwenyekiti wa na ataanza kazi kimataifa kwenda ofisi mbalimbali za kimataifa kwa ajili ya tukio la ukamataji wa Mwenyekiti huyo. Huku Mawakili wa ndani wataongozwa na Peter kibatala kufatilia jambo hilo kwa Dar es salaam.

Makamu Mwenyekiti, Mhe. John Heche ameyasema hayo akiongea na waandishi wa habari Songea Mkoani Ruvuma baada ya kukamatwa kwa Tundu Lissu bila kutolewa taarifa kuwa yupo wapi.

Tayari Jeshi la Polisi Tanzania limesema linamshikilia Tundu Lissu kwenye kituo kikuu cha Polisi (Central) Jijini Dar es salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *