Club ya Bayer Leverkusen imeshinda Ubingwa wa Ligi Kuu ya Ujerumani kwa mara ya kwanza katika historia yao baada ya kuifunga 5-0 Werder Bremen.
Bayer Leverkusen wanashinda Ubingwa huo wakiwa na michezo mitano imesalia mkononi kwani alama 79 walizonazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote hata kama watapoteza michezo yao mitano iliyobaki.
Leverkusen ni timu iliyoanzishwa miaka 120 iliyopita ndio kwa mara ya kwanza inatwaa Kombe hilo huku ikiwa na rekodi ya kucheza mechi 43 za mashindano yote bila kupoteza na kufanikiwa kumaliza ubabe wa Bayern Munich wa kutwaa Bundlesliga kwa miaka 11 mfululizo.
Kwa mara ya kwanza katika miaka 119 ya kuwepo kwa klabu, Bayer 04 Leverkusen ni mabingwa wa Bundesliga baada ya katika misimu kadhaa kupambania kombe hilo na kuishia katika nafasi ya pili na hiyo ilikuwa ni katika misimu ya 1996/97, 1998/99, 1999/00, 2001/02, 2010/11 na 2023/24.
Ni kama vile kocha Xabi Alonso amemaliza laana ya kutotwaa kombe hilo kwa Bayer Leverkusen katika msimu wake wa kwanza wa ukocha katika klabu hiyo.