Kuna haja ya kumsaidia Chid Benz- Haji Manara

Mwanamitandao na mfanyabiashara Haji Manara ameweka wazi kuumizwa na hali ya sasa ya msanii wa Muziki Chid Benz, ambapo amesema kuna haja ya kumsania msanii huyu anayetajwa kurudia kutumia madawa ya kulevya.

“Nimeona mitandaoni kuhusu lawama nyingi tunazopeana za kutomsaidia Msanii Chid Benz, kutokana na hali anayopitia ya Matumizi ya Uraibu anaoutumia.

Kwanza niseme mimi ni mshabiki mkubwa sana wa Chidi ,na Style yake ya kurap ilinipa wakati mzuri wa kuenjoy maisha miaka ile, kisha ni Mtoto wa kiswahili kama nilivyo mimi, Tumetokana na Hasslers na tunastahili kusaidiana hata kama tumeteleza!!

Najua Watu kadhaa washajaribu kumsaidia lakini bado hajakaa sawa, nipo tayari kumsaidia ,kuondokana kabisa na tatizo lake la kutumia Uraibu wake.

Raha yangu ni kumuona anarejea kwenye hali yake kama zamani, ni mtu talented kweli kweli, Kisha Mwana wa kitaa, uwezo wangu mdogo unaniambia naweza kusaidia na am ready.

Gharama zote za Rehab ikiwa ni pamoja na malazi, Chakula na matibabu ntazibeba, aje tu Wiki ijayo @manaratv__ Samora Avenue Salamander Tower.

Kuna Clip nimeiona mchana huu mitandaoni ikitembea imenichona na nadhani kuna haja ya kumsaidia very serious.

Sijui nampata wapi Shujaa wangu huyu lakini mpeni salaam zangu, Mwambieni kaka yako Haji amepata shauku kubwa ya kukusaidia, ningeweza kuifanya kimya kimya lakini nampatia wapi Chidi?”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *