KONGAMANO LA ELIMU MTANDAO AFRIKA LIMEONGEZA CHACHU MATUMIZI YA TEKNOLOJIA –KATIMBA


Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Zainab Katimba amesema kongamano la Kimataifa la Elimu Mtandao Afrika limeongeza chachu ya matumizi ya teknolojia ya katika ufundishaji ambayo ndio hitaji la dunia kwa sasa.

Katimba amesema hayo katika kongamano hilo lililofanyika katika ukumbo wa JNICC jijini Dar Es Salaam na mgeni rasmi akiwa ni Dkt. Doto Biteko, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati akimuwakilisha Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizungumzia hatua iliyofikiwa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI katika matumizi ya Taknolojia Mhe. Katimba amesema kwasasa serikali inafanya majaribio ya matumizi ya shule janja katika shule za sekondari za Kibaha na Dodoma ambayo Mwalimu anaweza akawa Kibaha akafundisha wanafunzi wa Dodoma kwa njia ya video.

“kwenye shule zetu tuna maabara na vifaa mbalimbali vya TEHAMA kwaajili ya kuwawezesha waliu wetu kufundishia na mpaka wakati huu tumeanza kufanya majaribio katika ya Teknolojia ya madarasa janja na tuko katika hatua ya majaribio Mwalimu akiwa anafundisha Kibaha kuna shule zingine zinaweza kujiunga kwenye darasa hilo na wakawa wanafanya ufundishaji mubashara,” amesema.

Aidha, Katimba amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inafanya mambo makubwa katika uwekezaji wa matumizi ya TEHAMA kuanzia shule za msingi na Sekondari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *