KIA KUFUNGWA KWA MATENGENEZO, MAGARI KUTUMIA NJIA MBADALA

Moshi, 28 Machi 2025 – Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Kilimanjaro imetangaza kufungwa kwa barabara kuu ya Himo – Njia Panda – Moshi – KIA Njia Panda kuanzia tarehe 28 Machi 2025 ili kuruhusu matengenezo katika eneo lililo karibu na Mzunguko wa Arusha (Arusha Roundabout).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Kilimanjaro, sehemu ya barabara hiyo imeharibika kutokana na uwepo wa bomba kubwa la maji safi chini ya njia hiyo.

Kutokana na hali hiyo, magari makubwa ya mizigo yenye uzito wa zaidi ya tani 10 yanashauriwa kutumia barabara mbadala ya Lucy Lameck – Ghala – Viwanda – Manyema – Mafuta – Nyerere – Bonite – Khambaita.

Kwa magari madogo, barabara mbadala ni kupitia YMCA – Kilimanjaro kupitia Bustani Alley.

Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) inawaomba radhi watumiaji wa barabara kwa usumbufu wowote utakaojitokeza wakati wa matengenezo haya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *