Kiongozi wa kisiasa wa kundi la waasi la M23 Corneille Nangaa amesema baada ya kuuteka mji wa Goma kazi iliyobaki ni kuingia Kinshasa.
Nangaa, alitangaza nia yake hiyo akisema sasa wanaelekea mji mkuu wa Kinshasa, kwa lengo la kuipindua serikali ya Rais Félix Tshisekedi ambaye naye alitoa wito kwa Vijana kujiunga na Jeshi ili kuingia kwenye mapambano.
Waziri wa Ulinzi wa Kongo, Guy Kabombo Muadiamvita alitoa maagizo kuwa mipango ya mazungumzo yoyote na waasi isitishwe na kwamba hawatakubali kushindwa.

Amesema, “tutakaa hapa Kongo na kupigana. Ikiwa hatutaishi hapa, basi tutaishi wafu hapa,” alisema Muadiamvita.
Kwa upande wake Rais Felix Tshisekedi aliwataka wananchi wa mashariki mwa nchi yenye rasilimali nyingi kukataa kukubali kutekwa kwa maeneo zaidi na wapiganaji hao.