Mwanamke mwenye umri wa miaka 35, aliyetambulika kwa jina la Myra Carvalho amehukumiwa kifungo cha wiki 14 jela kwa kosa la kumtumia kadi za salamu zipatazo 8,000 msanii wa muziki Harry Styles.
Mwanamke huyo anadaiwa kumtumia kadi hizo nyota huyo ndani ya mwezi mmoja kabla ya kuhukumiwa katika Mahakama ya Harrow Crown Jumanne ya wiki iliyopita.