Jambo Xtreme Watua Pamba Jiji.. Jamukaya Ramadhan Cup Kitawaka

Muwakilishi wa makampuni ya Jambo Group ambae ndiye mdhamini mkuu wa timu ya Pamba Jiji Fc kupitia kinywaji chetu cha JAMBO EXTREME POWER PLUS bwana Musa Ryoba siku ya jana tarehe 30/03/2024 akiwa na Naibu Meya wa jiji la Mwanza ambae pia ni Mwenyekiti wa Pamba Jiji Fc Bwana Biku Kotecha wakiteta jambo mara baada tu ya kumalizika kwa mchezo kati ya Pamba Jiji Fc na Police Tanzania.

Habari za upupu zinaonyesha kuwa, matembezi haya yaliyofanywa na Bwana Musa Ryoba yanalengo la kusaka vipaji vipya vitakavyo sajiliwa kwenye timu ya mpira ya Jambo Extreme Energy inayo shiriki mashindano ya Jamukaya Ramadhan Cup, ambayo kuanzia wiki hii yanaanza rasmi hatua ya robo fainali.

Mpaka sasa tukiwa tunaelekea mwishoni mwa ligi ya NBC Championship timu ya Pamba jana iliibuka na ushindi mnono dhidi ya Police Tanzania ikiwa katika uwanja wake wa Nyamagana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *