Serikali ya Tanzania imekubali kugharamia safari ya Mashabiki wa Yanga kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa robo fainali ta Klabu Bingwa Afrika utakaochezwa na Mamelod Sundowns.
Wizara imegharamia Mashabiki 48 ambao watakwenda Afrika Kusini kuisapoti timu siku ya Ijumaa ya April 4 2024 kwa usafiri wa basi, hili limefanyika baada ya Yanga kuiomba sapoti Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.