IFAHAMU OPARESHENI TATA YA MKONO KUUNGWA KWENYE MGUU

Desemba 17, 2013, Mfanyakazi mmoja wa kiwanda wa China anayeitwa Xie Wei alipitia utaratibu wa matibabu wa kushangaza ili kuokoa mkono wake uliokatika.

Hilo lilimtokea baada ya kupata ajali mbaya, ambapo Madaktari walifanikiwa kuuweka mkono wake ili usiharibike na uwe hai kwa kuushikanisha kwa muda kwenye kifundo cha mguu wake wa kushoto, wakitumia mishipa ya damu kutoka kwenye mguu wake.

Alikuwa ni Daktari Tang Juyu, ni mtaalamu wa kesi ngumu za kutengeneza tishu na majeraha. Kabla ya Xie kwenda kwenye upasuaji, Tang alimwambia kuwa alikuwa na matumaini na alitabiri kwamba angeweza kutumia tena mkono wake.

Tang aliamua njia bora ya kuokoa mkono huo ni kuushikamanisha na mguu wa Xie ambapo kulikuwa na ugavi mzuri wa damu. Mkono ungehitaji kukaa hapo hadi mkono wa Xie upone kabisa.

Hata hivyo, inaarifiwa kuwa hilo lilifanikiwa licha ya kuwa ulikiwa umekufa ganzi kabisa na hakuna uunganishwaji mwingine uliofanywa isipokuwa ile mishipa ya damu pekee.

Mhanga Xie alisema mguu wake alikiwa akihisi upo kawaida, ingawa alihisi uzito kidogo kuliko kawaida.

Mwezi mmoja baadaye, Madaktari wa upasuaji walifanikiwa kuunganisha tena mkono wake uliokatika kwa mafanikio.

Hata hivyo, naada ya Xie kutoka Hospitalini, aliweza tu kuuzungusha mkono wake kidogo lakini hakuweza kuchezesha vidole vyake.

Madaktari walimwambia itachukua karibu miezi sita kwa mishipa kupona na kwa matumaini yake ikiwemo mazoezi angeweza kuufanyisha kazi kikamilifu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *