‘HUWEZI KUENDESHA WATU WAKATI WOTE’ – MAKAMU WA RAIS YANGA

Makamu wa Rais wa Klabu ya Yanga, Arafat Haji kupitia akaunti yake ya Instagram ameandika ujumbe ambao umewatafakarisha wadau wengi wa michezo hasa kwenye kipindi hiki ambacho kumeibuka sintofahamu baada ya mechi ya Yanga na Simba kutochezwa.

Arafat ameandika “Unaweza kuendesha Watu ila huwezi kuwaendesha wakati wote, unaweza kuburuza watu ila huwezi kuwaburuza wakati wote, unaweza kuwaongopea watu ila huwezi kuwaongopea wakati wote, kuwa makini na maji yaliyotulia, yana kina kirefu sana”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *