HOSPITALI YA MIREMBE INAHUDUMIA WAGONJWA WOTE.

Watanzania wametakiwa kutambua kuwa Hospitali ya taifa ya Afya ya akili Mirembe inatibu magonjwa yote kama zilivyo hospitali zingine na siyo matatizo ya afya ya akili pekee kama wengi wanavyodhani.

Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki hii na Afisa habari na mahusiano kwa Umma kutoka hospitali hiyo Christian Alais wakati akifanya mahojiano maalum na Jambo FM wilayani Kahama mkoani Shinyanga katika kilele cha kangamano la afya ya akili.

Alais Amesema kuwa hospitali ya taifa ya akili  Mirembe ina wataalamu wabobevu wa masuala ya tatizo la afya ya akili ndiyo mana imeteuliwa kwa ajili ya kusaidia watu hao lakini magonjwa yote ya binadamu yanatibiwa katika hospitali hiyo.

“Hospitali ya Mirembe inatoa huduma za matibabu ya magojwa yote,tunatibu mifupa, Kinywa, Huduma za wagonjwa wa nje (OPD) na mengine Mengi,Ila swala la afya ya akili ni hospitali ya Mirembe pekee ndiyo imetuliwa kutibu watu wenye matatizo ya afya nchini” Amesema Alais.

Sambamba na hayo Alais ametoa wito kwa jamii kujitokeza Kwenda kupata matibabu mbalimbali katika hospitali ya Mirembe na kuacha tabia ya kuwaficha ndani watu wenye matatizo ya akili.

“Jitokezeni kutibiwa kwenye hospitali ya Taifa ya afya ya akili Mirembe,lakini pia msiwafiche watu wenye matatizo ya akili ndani,waleteni wapate matibabu” Amesisiza Alais.

Ameongeza kuwa lengo la Serikali ni kubadilisha jina lilipo kwa sasa la hospitali ya taifa ya afya ya akili na kuitwa taasisi ya taifa ya afya ya akili Tanzania na kwamba huduma zitaongezeka zaidi katika taasisi hiyo.

“Jina Mirembe limekaa kinyanyapa lenyewe tu sasa kwa zaidi ya miaka ishirini serikali ina mpango wa kulibadilisha jina hilo na itaitwa Taasisi ya taifa ya afya ya akili na huduma pia zitaongezeka katika taasisi hiyo” Ameongeza Alais.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa manispaa ya Kahama wameishukuru hospitali ya taifa ya afya ya akili Mirembe kwa kuwapa elimu hiyo kwani wengi wao walikuwa wakifahamu hospitali ya Mirembeni kwa ajili ya watu wenye matatizo ya akili tu.

“Kwakweli tunashukuru sana kwa elimu hii aliyotupatia afisa wa Mirembe,kwakweli tulikuwa hatujui kwamba hospitali hiyo inatibu magonjwa yote ila sasa tumejua” Amesema Bi Rehema Sadick.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *