
Makamu Mwenyekiti wa Chama ACT Wazalendo ambae pia ni Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman akiwa kwenye Ziara ya Kichama Pemba amesema kuna idadi kubwa wananchi Visiwani humo wamekosa Haki yao ya Msingi ya kujiandikisha kwenye Daftari
Omo amesema Wananachi wapatao 772 wamenyimwa haki yao na fursa ya kujiandikisha katika daftari la wapiga kura kwa upande wa pemba huku akisistiza kua hayo yalifanywa kwa makushdi
“Watu wapatao 772 wamenyimwa fursa ya kuandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa upande wa Pemba na haya yalifanywa kwa makusudi zaidi ya wananchi wapatao 772 , hatutakubali kwenda kwenye uchaguzi kwa mazingira haya—-Makamu Mwenyekiti Taifa Act Wazalendo “
Nae Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Act Wazalendo Ismail Jussa amesema Chama hicho hakipo pemba kutafuta nafasi za Ubunge na Uwakilishi
“Hatupo hapa kumtafutia mtu ama watu Ubunge na Uwakilishi, kama kuna mtu anadhani sisi tunaendeleza harakati hizi kwa sababu ya yeye ama wao kutafuta kijio basi tunasema wazi kuwa mtu huyo hatufai na mlango upo wazi–Jussa Makamo Mwenyekiti Act “